Mahakama yaamua matokeo katika vituo vya kupigia kura ni sahihi

Mahakama ya rufaa imeamua kuwa matokeo ya urais yatakayotangazwa katika maeneo bunge ni ya mwisho na hayawezi kubadilishwa au kukarabatiwa, ila tu kufuati agizo la mahakama. Majaji watano wa mahakama ya rufaa wametupilia mbali kesi iliyowasilishwa na tume ya uchaguzi nchini-IEBC, na kusisitiza mabadiliko yaliyofanywa kwenye sheria za uchaguzi yanazuia udanganyifu au jaribio lolote la afisa wa uchaguzi mkorofi kuyapiga msasa matokeo. Huku kesi ya IEBC ikipigwa teke, kinara wa NASA Raila Odinga na kikosi walikuwa na tabasamu si haba, huku wakidai uamuzi wa leo ni tiba tosha dhidi ya wizi wa kura.

Tags:

IEBC Wafula Chebukati mahakama ya rufaa kura ya urais Matokeo ya kura

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories