Mahakama yaruhusu NASA kukagua mitambo ya IEBC japo kwa masharti


Mawakili wa viongozi wa Nasa Raila Odinga na Kalonzo Musyoka na wale wa Rais Uhuru Kenyatta wanapekua stakabadhi na mitambo ya teknolojia iliyotumiwa katika uchaguzi uliofanyika terehe nane mwezi huu. Haya ni baada ya kupata ruhsa kutoka kwa mahakama ya kilele mbapo agizo lilitolewa kuwa shughuli hiyo ambayo inasimamiwa na msajili wa idara ya mahakama ikamilike na ripoti kuwasilishwa kufikia saa kumi na moja jioni hapo kesho.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Faiza Wanjiru
More by this author