Mahakama yatupilia mbali kesi ya Nasa dhidi ya mfumo mbadala wa uchaguzi
Mahakama Kuu imetupilia mbali kesi ya muungano wa upinzani NASA iliyonuia kusimamisha uchaguzi ujao endapo mfumo wa kielektroniki wa kuandaa uchaguzi ungefeli. Majaji watatu wa mahakama hiyo wanasema tume ya uchaguzi iko huru kuandaa mfumo mbadala kuandaa uchaguzi huo ili kujiandaa kutokana na hitilafu za mitambo. Haya yanajiri huku IEBC ikizidisha maandalizi ya uchaguzi tume hiyo ikijiandaa kufuatana na washikadau mbalimbali kuelekea Dubai kukagua shughuli ya uchapishaji wa karatasi za kupigia kura ya urais.
Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke
Comments
No comments yet.
Leave a Comment