Makachero wanachunguza kifo cha Nkaissery

Uchunguzi umeanzishwa kubaini kilichosababisha kifo cha waziri wa usalama wa kitaifa Joseph Nkaissery usiku wa kuamkia leo, na kuligubika taifa na wingu la simanzi. Upasuaji na uchunguzi wa maiti ya mwendazake unatarajiwa kufanyika kati ya kesho na Jumatatu, huku wataalam wa upekuzi wakizuru mkahawa wa Bomas alikozuru mwendazake na kushiriki kinywaji, nyumbani kwake mtaani Karen na hifadhi ya maiti ya Lee, kukusanya chembe chembe muhimu zitakazoweza kukitegua kitendawili cha kifo chake. Haya yanajiri, huku Rais Uhuru Kenyatta akimteua waziri wa elimu Dkt. Fred Matiang’i kushika doria katika wizara ya usalama kwa muda.

Tags:

NIS CID Nkaissery

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories