Maraga: Kulikuwa na kasoro katika mchakato wa uchaguzi


Mahakama ya upeo imeelezea kwa kina sababu za kubatilisha uchaguzi wa Rais Uhuru Kenyatta, huku ikiorodhesha msururu wa dosari za tume ya uchaguzi-IEBC katika maandalizi ya mchuano huo. Jaji mkuu David Maraga, naibu wake Philomena Mwilu, majaji Isaac Lenaola na Dkt Smokin Wanjala waliinyoshea kidole cha lawama tume ya IEBC kwa kufeli kuhakiki stakabadhi za kuwasilisha matokeo ya kura, na kuafiki kuwa mitambo ya upeperushaji matokeo ilivurugwa, baada ya iebc kudinda kuifungua ili ikaguliwe kama ilivyoagizwa na mahakama.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Francis Gachuri
More by this author