Maraga: Tunaendelea kuandika uamuzi


Jaji Mkuu David Maraga anasema Majaji sita wa mahakama ya upeo wangali wanaandika uamuzi wao kuhusu kesi mbili zinazonuia kubatilisha uchaguzi wa Oktoba 26 uliompa Uhuru Kenyatta Ushindi. Akizungumza baada ya kuhudhuria ibada ya kanisani hapa Nairobi Maraga anasema watatoa uamuzi huo saa tano siku ya Jumatatu, majaji hao wakiaminika kuwa wanaandika uamuzi wa kila mmoja binafsi kabla ya kukutana kuwianisha misimamo.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: The Fresh Look 9PM Bulletins... #ThisIsTheStory

Story By Sam Gituku
More by this author