Marehemu Gavana Gakuru kuzikwa tarehe 18

Marehemu gavana wa Nyeri Gakuru Wahome huenda akazikwa tarehe kumi na nane mwezi huu, akipata mazishi ya kitaifa yatakayofadhiliwa na serikali. Waziri wa mawasiliano ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa kamati ya mazishi anasema uamuzi huo umeafikiwa kuambatana na hadhi ya Wahome huku maandalizi ya mazishi nyumbani kwake huko Nyeri yakianza. Haya yanajiri huku hafla ya kumwapisha naibu gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga ambayo ilitarajiwa kufanyika hapo kesho ikiahirishwa.

Tags:

Joe Mucheru nyeri Wahome Gakuru josephat nanok

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories