Marwa asema doria itaimarishwa Boni

Mratibu wa masuala ya usalama katika eneo la Pwani Nelson Marwa ametangaza kwamba serikali inapania kuongeza idadi ya maafisa wa usalama katika eneo la msitu wa Boni, Kaunti ya Lamu.
Kulingana na Marwa, hatua hiyo inalenga kupiga jeki juhudi za serikali za kupambana na visa vya ugaidi karibu na eneo hilo. Matamshi ya Marwa yakikuja siku moja baada ya gari la polisi kulipuliwa kwa kilipuzi kilichotegwa barabarani likiwa njiani kuelekea eneo la Kiunga ambapo watu wanane wakiwemo wanafunzi wanne na maafisa wa polisi wanne wameaga dunia hadi sasa.

Tags:

Al Shabaab Boni Forest Marwa pwani

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories