Mashambulizi yazidi Baringo

Senteiyo keiteiya, mtoto wa miaka sita tuliyemwangazia hapo jana akiuguza majeraha ya risasi  baada ya shambulizi la mukutani katika kaunti ya  Baringo, mamesafirishwa hadi hapa jijini nairobi kwa matibabu zaidi.

Msichana huyo aliyeponea shambulizi lililopelekea vifo vya watu 11 alinyimwa fursa ya matibabu katika hospitali moja ya kibinafsi mjini nakuru baada ya kukosa ada ya shilingi 20,000.

Huku akiendelea kupokea matibabu kwa hisani ya wafadhili waliojitokeza, wakaazi wa kijiji chake wanaendelea kuhamishwa katika maeneo salama kufuatia machafuko yanayozidi kushuhudiwa katika kaunti ya Baringo.

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories