Mashirika ya kiraia yamtaka Fazul Mohammed kujiuzulu

Serikali imeagiza kufungwa kwa shirika la africog, siku moja tu baada ya kubatilisha usajili wa shirika la kutetea haki za kibinadamu la kenya human rights commission (KHRC) na kuwaghadhabisha wanaharakati. Kando na kutaka wakurugenzi wa shirika la africog watiwe mbaroni na akaunti zake za benki kufungwa, bodi ya kuratibu shughuli za mashirika ya kijamii linashinikiza wafanyi kazi wote wa kigeni wanaohudumu katika shirika hili, na lile la khrc wafurushwe. Je, mjeledi wa serikali una uhusiano wowote na uwasilishaji wa kesi katika mahakama ya juu zaidi nchini, kupinga matokeo ya kura ya urais? Francis Gachuri ana taarifa kamili.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories