Mataifa ya Ulaya yasuta misimamo ya Nasa na Jubilee


Mataifa ya magharibi yakiwemo Marekani, Uingereza na Ujerumani yamevisuta vyama vya Jubilee na NASA kutokana na mtafaruku unaoendelea kuhusu maandalizi ya marudio ya uchaguzi wa urais ambayo sasa yanasalia na siku kumi na nane pekee. Katika taarifa zilizotumiwa vyombo vya habari, mataifa hayo yameutaka muungano wa NASA kusitisha matakwa yake dhidi ya IEBC wanayosema yanahujumu juhudi za tume hiyo kuandaa uchaguzi huku chama cha Jubilee kikisutwa kwa kubadilisha sheria za uchaguzi.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: | BULLDOZERS FOR SANITIZERS | Families remain in the cold after evictions from Kariobangi sewage estate

Avatar
Story By Sam Gituku
More by this author