Mawakili wa Uhuru wasema alishinda kwa haki


Rais Uhuru Kenyatta ameutetea ushindi wake katika mchuano wa ikulu ulioandaliwa tarehe nane mwezi huu na kusimamiwa na tume ya uchaguzi nchini-IEBC. Kenyatta kupitia kwa mawakili wake Fred Ngatia, Ahmednassir Abdulahi na Tom Macharia amesema kesi iliyowasilishwa na kinara wa Nasa Raila Odinga haina uzito wowote kisheria, wala ushahidi muafaka kuthibitisha madai ya wizi wa kura na udukuzi wa mitambo ya IEBC. Aidha, Kenyatta amesema kubatilisha ushindi wake ni sawa na kukiuka haki ya wakenya kuwachagua viongozi bila kushurutishwa.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Francis Gachuri
More by this author