Mawakili waovu waonywa

Jaji Mkuu David Maraga amekishurutisha chama cha wanasheria nchini kuweka adhabu kali kwa wanasheria wanaojihusisha na ukiukaji wa sheria.

Akizungumza katika hafla ya kuidhinisha wanasheria 123, jaji huyo alishikilia msimamo wake mkali dhidi ya kupigana na ufisadi. Itakumbukwa kuwa hiki ni kikundi chake cha kwanza kuidhinisha tangu alipopewa wadhfa kama jaji mkuu na kumridhi jaji mustaafu daktari willy mutunga.

Wakati huo huo ,aliongoza kikao maalum katika mahakama   kuu nchini kwa ajili ya kumkumbuka marehemu jaji mkuu mstaafu abdul majid cockar kama ilivyo desturi katika ulingo wa sheria.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories