Mbunge wa Laikipia kaskazini ashtakiwa kwa mauaji

Mbunge wa Laikipia kaskazini Mathew Lempurkel ameshtakiwa na makosa ya mauaji na uchochezi katika mahakama moja mjininanyuki kaunti ya Laikipia.

Mbunge huyo ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili na mdhamini wa kiasi hicho na kuagizwa kuwa mwenye kujiwasilisha katika makau makuu ya kitengo cha upelelezi kaunti ya Laikipia mara tatu kwa wiki.

Hatahivyo hali ya usalama ingali tete katika eneo hilo kwani lori moja lililokuwa katika shughuli ya kusafirisha mifugo wanaonunuliwa na serikali lilishambuliwa kwa risasi katika tukio lililokosa kumjeruhi yeyote.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories