Mbunge wa Nyeri mjini akubali kuondoa hoja ya kumtimua jaji mkuu

Mbunge wa Nyeri mjini Ngunjiri Wambugu ameshinikizwa kuondoa hoja aliyowasilisha jana ya kumng’atua Jaji Mkuu David Maraga ofisini kwa madai ya ukiukaji wa majukumu yake. Rais Uhuru Kenyatta, naibu wake William Ruto na vinara wa wengi katika bunge la kitaifa na seneti wamesema hoja hiyo, ingawa imeibua masuala mazito, sio ya dharura kwa sasa, huku mchuano mpya wa ikulu ukizidi kubisha hodi. Hata hivyo, suala ibuka ni je, hoja ya Wambugu ilikuwa kifunga macho cha kisiasa, ili kuziteka fikra na nyoyo za wenyeji wa eneo nzima la Kisii?

Tags:

Ngunjiri Wambugu Chief Justice Maraga Petition

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories