Mkahawa wa Jacaranda watimiza masharti ya usafi

Mkahawa wa Jacaranda umefunguliwa tena na kuruhusiwa kisheria kuendesha shughuli zake za kawaida, siku chache baada ya kufungwa kutokana na viwango vya chini vya usafi ili kuzuia maambukizi ya maradhi ya kipindupindu.
Naibu msimamizi wa masuala ya afya ya umma katika kaunti ya Nairobi ameeleza hatua hiyo na kukiri kuafikiwa kwa viwango vya afya vinavyotakikana.
Mawaziri cleopa mailu wa afya, Najib Balala wa utalii na Sicily Kariuki wa masuala ya vijana na jinsia walifika katika mkahawa huo mchana wa leo kujipatia chamcha ili pia kuonyesha kwamba kila kitu ki shwari kwenye hoteli hiyo.

Tags:

cholera kipindupindu Jacaranda

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories