Mkutano wa NASA Eldoret

Viongozi wa muungano mkuu wa upinzani NASA wamefanya mkutano wao wa kwanza katika uwanza wa 64 stadium mjini Eldoret katika kaunti ya Uasin Gishu.

Wakiongozwa na Raila Odinga, walihutubia mkutano na kusema kuwa NASA ikibuni serikali itatoa jawabu kwa masaibu ya wakenya ikiwemo kupambana na zimwi la ufisadi. Vijana wengi walijitokeza kuwasikiliza wanasiasa hao walioisuta serikali ya Jubilee wakidai kuwa imeshindwa kutimiza ahadi ilizotoa. Kadhalika hali ya maisha imekuwa ngumu na kwamba NASA ndio wana dawa. Viongozi hao wamewataka wakenya wasiwe na wasiwasi kuhusu atakayepeperusha bendera ya urais kwa tikiti ya NASA kwani jibu liko karibu kupatikana.

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories