Mkuu wa tume ya ardhi ajikuta pabaya

Kamati ya bunge kuhusu ardhi hii leo imekutana na waziri wa ardhi Jacob Kaimenyi kuhusu hoja ya kumngatua mamlakani kwa mwenyekiti wa tume ya ardhi nchini  Mohamed Swazuri. Kamati hiyo ilitaka kujua ukweli wa madai yaliyotolewa dhidi yake Swazuri yaliyowasilishwa na mwanabiashara Mugo Njeru. Kaimenyi alielezea kamati hiyo kuwa baadhi ya stakabadhi zilizowasilishwa ofisni mwake kuhusu ardhi iliyokuwa imezozaniwa katika eneo la Embakasi ni gushi. Kamati hiyo imekamilishwa mahojiano na wahusika wote na sasa imeanza kuandaa ripoti yake ya mwisho ya iwapo swazuri ataondoka ofisini au la.

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories