Moses Kuria na Muthama wakamatwa


Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria na aliyekuwa Seneta wa Machakos Johnstone Muthama wamekamatwa kwa madai ya kutoa matamshi ya chuki.

Wawili hao wamefikishwa katika makao makuu ya idara ya ujasusi nchini ambapo wamehojiwa kwa zaidi ya saa moja na makachero kutoka idara hiyo. Moses Kuria anatuhumiwa kueneza matamshi ya chuki  dhidi ya kiongozi wa Nasa Raila Odinga na familia yake  mbali na tuhuma za kuwataka watu zaidi ya laki moja waliopigia kura odinga kufurushwa kutoka kaunti hiyo.  Kwa upande wake Johnstone Muthama, inadaiwa alitoa matamshi ya chuki wikendi hii iliyopita kwenye mkutano wa kisiasa wa Nasa. Waziri wa usalama Daktari Fred Matiang’i amesisitiza kwamba wachochezi wote watakamatwa na kukabiliana na msumeno wa sheria.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

citizen
Story By Citizen
More by this author