Moto wateketeza sehemu kubwa ya msitu wa Aberdare

Sehemu kubwa ya msitu wa Aberdare imeteketea. Kulingana na maafisa wa huduma za misitu nchini KFS, moto huo ulizuka jana saa nne asubuhi na kusambaa kwa kasi kwa sababu ya upepo na hali kame.

Moto huo umezuka siku chache tu baada ya KFS kutoa tahadhari kuhusu uwezekano wa kuzuka kwa moto kutokana na upepo na jua kali.

Maafisa kutoka shirika la huduma kwa Misitu nchini wametumwa kutathmini kiwango cha uharibifu ambao umesababishwa na mkasa huo ambao unahofiwa kuathiri kiwango cha maji ya mito inayotoka kwenye milima ya Aberdare. Wananchi wametakiwa kuwa waangalifu kwani moto huo unaweza kusambaa zaidi.

Tags:

Aberdare msitu wa aberdare msitu wateketea

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories