Msamaria mwema apiga jeki elimu ya mtoto mlemavu huko Kwale


Hakuomba msaada, hakutaka kuhurumiwa, alijikakamua bila ya kujua kuna watu wanaomuona na kutaka kumpa asichoitisha ila anakihitaji. Ari yake na kiu ya elimu iliwavutia wahisani. Erick Mbithi Mwanafunzi Wa Darasa La Tano Mwenye Ulemavu Wa Miguu Kutoka Shule Ya Msingi Ya Msulwa ambaye alikuwa akitembea na kupanda milima akishuka mabonde ya shimba hills kaunti ya Kwale, kusaka elimu, sasa amepata mfadhili aliyeahidi kumlipia karo na kumhamishia Katika Shule Ya Uwezo Maalumu Ya Potreiz Katika Kaunti Ya Mombasa.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Nicky Gitonga
More by this author