Mshikuwa Feisal Mohammed Hatimaye Anaswa

Afisa mkuu wa kituo cha polisi cha Bamburi Inspekta Mkuu David Muli atakuwa wa kwanza kufunguliwa mashtaka chini ya sheria mpya za usalama. Afisa huyo atafikishwa katika mahakama ya mombasa kesho kuhusiana na sakata ya kutoweka kwa magari 16 yaliyokuwa yakizuiliwa kufuatia kunaswa kwa shehena ya pembe za ndovu katika mtaa wa Tudor huko Mombasa. Shehena hiyo inashirikishwa na mfanyibiashara wa Mombasa Feisal Mohammed ambaye amenaswa leo na maafisa wa Interpol kuhusiana na ulanguzi wa pembe za ndovu.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories