Mtahiniwa wa KCPE ateketeza nyumba za mama yake


Mtahiniwa wa KCPE ateketeza nyumba za mama yake
Fire. Photo/FILE

Mtahiniwa mwenye umri wa miaka 19 anafanya mtihani katika kituo cha polisi cha Bomet baada ya kukamatwa jana usiku kwa tuhuma za kuteketeza nyumba za mama yake katika kijiji cha Keliot.

OCPD wa Bomet Samson Rukunga amesema mshukiwa alikamatwa na wakaazi wenye ghadhabu, waliompeleka katika kituo cha polisi.

Mshukiwa huyo ni miongoni mwa wengine 27 waliosajiliwa kama watahiniwa binafsi wanaofanya mtihani katika shule ya msingi ya Bomet.

Mkurugenzi wa elimu katika kaunti hiyo Indianzi Mabale amesema mshukiwa yuko mikononi mwa polisi na atafanya mtihani kufuatia utaratibu utakaowekwa na maafisa hao.

Aidha Rukunga amesema mwanafunzi huyo atakamatwa tena baada ya mtihani na kushtakiwa kwa kuhatarisha maisha ya Mamake mbali na kuharibu mali.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: CAS Rachel Shebesh and athlete Asbel Kiprop share their mental health journeys

Citizen Reporter
Story By Citizen Reporter
More by this author