Mtu mmoja auwawa kwenye msafara Baringo

msafara uliokuwa ukisafirisha miili ya wahasiriwawa  9 walioangamia wiki jana katika ajali kwenye barabara ya Marigat-Loruk huko kapedo, ulivamiwa katika barabara hiyo hatari inayokumbwa na mashambulizi ya kila mara, hali iliyosababisha kifo cha mmoja wa waombolezaji,na kulazimu  polisi waliojihami wapelekwe kutoa usalama kwa msafara huo.

 

Shambulizi hilo lilitokea kilomita chache kutoka kambi ya wanajeshi KDF eneo la Chesitet   baada ya Msafara huo uliokuwa ukisafirisha maiti hizo  kushambuliwa   jambo ambalo lilipelekea  ulinzi kuimarishwa.

Hafla ya mazishi ya wahasiriwa  19 wa ajali, ambayo ilihudhuriwa na viongozi kadhaa akiwemo gavana wa Turkana, Josphat Nanok, ilishuhudia lawama zikielekezwa kwa serikali kwa kushindwa kumaliza ujambazi na mashambulizi ya mara kwa mara kati ya jamii jirani za Pokot na Turkana.

Gavana Nanok ambaye pia alipoteza jamaa zake katika ajali hiyo, ametoa wito kwa bunge la Senate kuharakisha kupitisha mswada unaolenga kusuluhisha mizozo ya kila mara huko Kapedo kati ya wapokot na wakaturkana.

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories