Mudavadi ashabikia hatua ya kuunda muungano mkuu

Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi ameshikilia kuwa hajajiunga na CORD ili kuunda muungano maalum bali ni kuwa vyama vya upinzani vitakuja pamoja kama washirika sawa kwenye mikakati ya kumfurusha Rais Uhuru Kenyatta na Naibu Rais William Ruto kutoka mamlakani. Mudavadi anasema kuwa muungano huo haujachochewa na nyadhifa wanazotafuta vinara wake bali ni kwa minajili ya kumchagua mmoja wao kuwa mgombea urais na wengine kuleta kura zao pamoja kuhakikisha kuwa watakayemteua atapata ushindi kwenye uchaguzi wa mwaka ujao.

Tags:

CORD raila odinga Musalia Mudavadi ANC Super Alliance

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories