Mume wa bingwa wa mbio za mita 5000 azungumza

Familia ya mwanariadha Vivian Jepkemoi Cheruiyot inasherehekea ushindi wake wa mbio za wanadada za mita 5000 katika michezo ya olympiki inayoendelea nchini brazil. Akizungumza nyumbani kwake hii leo, mumewe Cheruiyot, Moses Kiplagat alionyesha furaha yake baada ya mke wake kunyakua medali yake ya kwanza ya dhahabu na kulipatia taifa hili medali ya tano katika michezo hiyo. Aidha Kiplagat ameelezea kuwa alitarajia ushindi huo huku akitaja maandalizi kabambe kama siri ya ushindi wa mkewe.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories