Muungano wa NASA uliwasilisha kesi mahakamani jana


Kinara wa NASA Raila Odinga usiku wa jana aliwasilisha kesi katika mahakama ya juu zaidi nchini, kupinga uchaguzi wa Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake kuhudumu kwa muhula wa pili. Odinga, katika ombi lake lenye zaidi ya kurasa 25,000 kwa majaji saba wa mahakama hiyo, anashinikiza matokeo ya mchuano wa urais yabatilishwe na uchaguzi mpya kuandaliwa. Francis Gachuri ana taarifa kamili kuhusu kesi ya NASA.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Francis Gachuri
More by this author