Mvutano kuhusu maji Muranga

Mvutano kuhusu maji Muranga

BY Steve Shitera

Malumbano kati ya gavana wa Murang’a Mwangi wa Iria na mwenzake wa Nairobi Mike Sonko kuhusu maji ya Ndakaini yanazidi kuchacha huku gavana Wa Iria akisisitiza kuwa hatalegeza kamba kwa kudai asilimia 25 ya malipo ya maji ya ndakaini yanayotumiwa na wakaazi wa Nairobi.

Hii leo serikali ya kaunti ya Murang’a iliandaa vikao na wananchi wa eneo hilo kutafuta maoni yao kuhusu maji yaliyozua utata baina ya kaunti za Nairobi na Murang’a.

Gavana wa Iria amesisisitiza kuwa lazima vipengee kwenye katiba vibadilishwe ili raslimali za kaunti kama vile maji na mafuta ziwafaidi wenyeji.

Wakaazi nao walitoa hisia zao huku wakilalamikia kukosa maji nyumbani  ilhali maji hayo yanatoka kwenye kaunti  yao na kufaidi pakubwa kaunti jirani hata wakipendekeza serikali ya muranga kutoza maji hayo ushuru.

Lakini wafanyi biashara jijini wamepinga madai ya gavana wa muranga  wakisisitiza kuwa lazima kuwe na mazingira bora ya kufanya biashara.

Aidha wamewarai magavana hao wawili kuweka kando tofauti zao na kuweka mikakati ya kuwafaidi wenyeji wa kaunti hizi mbili.

Pia wamewataka magavana sonko na wa iria kuheshimu mwongozo alitoa raisi siku mbili zilizopita kuhusu maji hayo yenye utata.

Rais alisema maji hayo ni raslimali ambayo haipasi kuingizwa katika siasa.

Tags:

muranga

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories