Mwanafunzi anayedaiwa kuwasha moto shule ya Moi ashtakiwa


Mahakama ya watoto imeruhusu maafisa wa upelelezi wanaoendeleza uchunguzi wa mkasa wa moto katika shule ya upili ya wasichana ya Moi hapa jijini Nairobi kumzuilia mshukiwa mmoja kwa siku saba wanapoendeleza uchunguzi. Mshukiwa ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza atazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kilimani hadi Jumatano ijayo huku maafisa wakipekuapekua baadhi ya ushahidi walionao zikiwemo simu yake ya rununu na kipakatalishi, zilizochukuliwa nyumbani kwao hiyo jana.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Hassan Mugambi
More by this author