Mwanamke mmoja anauguza majeraha ya macho baada ya kudhulumiwa na mumewe

Mwanamke mmoja anauguza majeraha ya macho baada ya kudhulumiwa na mumewe kufuatia mzozo wa shilingi 150 alizompa kununua chakula. Inadaiwa Irene Atieno alivamiwa na mumewe baada ya kudai fedha zaidi akisema kuwa alikuwa anunue vyakula zaidi kwa nyumba pamoja na kumnunulia mwanao dawa

 

Irene Atieno sasa atasalia na jicho moja tu hii ni baada ya mumewe rashid wanyonyi ambaye pia ni fundi katika mji wa kimilili kumdhulumu na kumjeruhi vibaya kwenye jicho lake la kulia pamoja na kumpelekea kupoteza meno tatu. Sababu kuu ya ugomvi uliompelekea Wanyonyi kumdhulumu mkewe ikiwa ni kuitishwa fedha zaidi baada ya kumpa shilingi 150 kumnunulia mwanao dawa pamoja na kununua bidhaa za nyumba. Kwa sasa Atieno ambaye daktari wamesema kuwa hana uwezo wa kuona ameitaka serikali kuingilia kati na kumwezesha kupata haki     

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories