Mwawakili wa Rais Kenyatta kutoa majibu kwa mahakama Jumatatu


Mawakili wa tume ya uchaguzi nchini-IEBC na wake wa Rais Uhuru Kenyatta hapo kesho wanatarajiwa kuwasilisha stakabadhi katika mahakama ya upeo, kujibu mashtaka ya John Harun Mwau, Njonjo Mue na Khelef Khalifa wanaotaka matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwezi jana yatupiliwe mbali na zoezi jipya kuandaliwa. Mchana kutwa, mawakili hawa wamekuwa kwenye pilka pilka za kuwianisha hoja zao, huku dkt. Ekuru aukot, aliyewania urais mwezi jana na kubwagwa akiwasilisha ombi la kujumuishwa kwenye kesi hizo mbili.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: Viusasa is now better, enriched with content and cheaper

Story By Francis Gachuri
More by this author