Mwili wa rubani waletwa Nairobi kwa uchunguzi

Idara ya kuchunguza ajali za ndege imeanzisha uchunguzi ili kubaini chanzo cha kisa ambacho ndege moja ilianguka katika ziwa Nakuru na kuwaacha watu watano kufariki.
Kwa mujibu wa mchunguzi mkuu wa idara hiyo, Martyn Lunani, tayari mwili uliobainika kuwa wa rubani Apollo Malowa umesafirishwa hadi Nairobi kwa uchunguzi kabambe.
Aidha Lunani anasema kuwa habari kuhusu jinsi ndege hiyo ilivyotua angani pamoja na data muhimu kuhusu utendakazi wake utabainika punde tu mabaki yote ya ndege hiyo itakapopatikana. Ndege hiyo ilianguka katika ziwa Nakuru siku ya Jumamosi, mda mchache tu baada ya kupaa kutoka hoteli ya jarika.

Tags:

Amboseli APOLLO MALOWA Nakuru helicopter crash

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories