Mzozo wa kidiplomasia unatokota katika ya Kenya na Tanzania

Serikali ya Kenya imetoa malalamishi rasmi kwa serikali ya Tanzania, kufuatia uamuzi wa kuwanadi zaidi ya ng’ombe 1,300 wa wafugaji kutoka kaunti ya Kajiado waliovuka mipaka kuwatafutia lishe. Waziri wa mashauri ya kigeni Amina Mohamed amesema serikali ya Kenya imelichukulia suala hilo kwa uzito, kwani linadhoofisha uhusiano wa mataifa haya mawili, na kutatiza juhudi za utangamano wa eneo la Afrika Mashariki. Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesisitiza hamna lolote la kujutia, na kuwa mifugo wa Kenya watakaovuka mipaka, wembe utakuwa ule ule.

Tags:

kenya Tanzania Maasai John Pombe Magufuli Kenya-Tanzania diplomatic row

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories