Nasa yafika Tharaka Nithi

Vinara wa muungano wa upinzani-nasa wamehitimisha ziara yao ya siku mbili katika kaunti za meru na tharaka nithi, iliyolenga kuwarai wenyeji kubadili mkondo kisiasa, kwa madai ya serikali ya Jubilee kushindwa kutimiza ahadi ilizotoa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2013.

Viongozi wa nasa raila odinga na kalonzo musyoka wamewahimiza wakazi wa eneo la mlima kenya kupiga darubini utendakazi wa Jubilee, huku wakitilia shaka uwezo wa Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kupunguza gharama ya maisha, kuimarisha uchumi wa taifa na kukabiliana na tatizo la ukosefu wa usalama.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories