NASA yaishtaki IEBC

Muungano wa upinzani-NASA umewasilisha keshi mahakamani, kupinga utoaji wa zabuni ya kuchapisha karatasi za kupiigia kura kwa kampuni ya Al-Ghurair, yenye makao yake mjini Dubai. Jopo la mawakili wa NASA linaitaka mahakama kuu kubatilisha zabuni iliyopewa kampuni hiyo, na kuagiza isihusishwe kwenye zoezi jipya la kuamua atakayechapisha karatasi hizo  zitakazotumika mwezi Agosti. Hata hivyo, Jubilee imekashifu hatua ya NASA na kuitaja kama ishara ya kuhofia kubwagwa kwenye debe, huku jaji mkuu David Maraga akiahidi maamuzi ambayo hayatavuruga maandalizi ya uchaguzi mkuu.

Tags:

IEBC raila odinga NASA Al Ghurair Ballot printing tender

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories