NASA yashutumu IEBC kwa madai ya kupuuza mapendekezo yao


Huku mkutano kati ya muungano wa Nasa na tume ya uchaguzi ukitibuka baada ya Nasa kususia mkutano huo, muungano wa Nasa sasa unasema kuwa haukualikwa kwenye mkutano wowote na kuwa haitafanya mikutano na IEBC ila itahusika tu kwenye mkutano wa kitaifa wa wadau. NASA inalalamika kuwa tume ya uchaguzi inapuuza mapendekezo iliyotoa na upungufu uliotajwa na mahakama ya upeo ili uchaguzi uwe huru na wa haki.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Faiza Wanjiru
More by this author