Nasa yazidi kujiimarisha Ukambani


Muungano wa Nasa umejizatiti kushikilia ngome zao ambapo wanawarai wafuasi wao kujitokeza kwa wingi katika marudio ya uchaguzi ili kuwapa Raila Odinga na Kalonzo Musyoka ushindi. Viongozi hao ambao walikuwa katika kaunti ya Machakos hii leo walitaja eneo hilo kama moja wapo ya maeneo ambapo kura zao za urais na ugavana ziliibiwa. Aidha wamewataka wafuasi wao kusimama imara na kutoshurutishwa na wale ambao wamehamia Jubilee baada ya kushindwa.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Faiza Wanjiru
More by this author