Nkaissery Ahojiwa Bungeni

Itajulikana wiki ijayo iwapo Joseph Nkaissery ataungwa mkono au la na kamati ya uteuzi ya bunge kuchukua wadhfa wa waziri wa usalama. Kamati hiyo inaoongozwa na spika wa bunge Justin Muturi leo imemfanyia Nkaissery mahojiano na inatarajiwa kuandaa na kuwasilisha ripoti yake bungeni kuanzia jumanne wiki ijayo. Nkaissery alihitajika kuelezea mbele ya kamati hiyo namna atakabiliana na ukosefu wa usalama nchini na pia ufisaadi kwenye wizara ya usalama. Wabunge pia  walimuuliza masuali kuhusiana na operesheni ya kupokonya silaha aliyosimamia huko Pokot mwaka wa 1994 ambako ilidaiwa kulikuwa na ukiukaji wa haki za binadamu.

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories