Nyongo na Outa watetea vijana waliokamatwa kwa kuzua fujo Kisumu

Seneta wa Kisumu Anyang Nyong’o na mbunge wa Nyando Fred Outa hawakuweza kuwashawishi polisi kuwaachilia vijana saba ambao wamezuiliwa kwa madai ya kuvuruga shughuli katika afisi ya gavana wa Kisumu Jack Ranguma. Vijana hao saba walitiwa mbaroni siku ya juma nne na kufikishwa mahakamani hapo jana ambapi jaji aliwaruhusu polisi kuwazuiliwa vijana hao kwa siku saba hadi pale uchunguzi utakapokamilika.
Kulingana na maafisa wa polisi, baadhi ya waliotiwa mbaroni ni vijana wanaodaiwa kuhusika na kundi haramu la China Boys tuhuma ambazo viongozi hao walipuuzilia mbali wakisema kuwa makundi ya American Marine na China Boys hawapo tena kisumu.
Mahakama ya kisumu itatoa uamuzi wao siku ya Jumatatu.

Tags:

kisumu Anyang Nyongo Fred Outa Jack Ranguma

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories