NYS Waondoa Vifusi Vya Ukuta Uliobomolewa, Langata

Wizara ya ardhi pamoja na tume ya ardhi kwa ushirikiano na shirika la vijana wa huduma kwa taifa NYS mapema leo ilianza zoezi la kutoa vifusi vya ukuta uliobomolewa siku ya jumatatu na wanafunzi wa shule ya msingi ya Langata road wakilalamikia unyakuzi wa ardhi yao. Haya yanajiri baada ya waziri wa usalama Joseph Nkaissery hapo jana kumpa mstawishaji aliyekuwa amejenga ukuta huo saa 24 kuondoa vifusi hivyo. Isitoshe, waziri wa ardhi Charity Ngilu na mwenyekiti wa tume ya ardhi Muhammad  Swazuri leo wamezuru maeneo mbali mbali hapa Nairobi ambako kumekuwepo na madai ya  unyakuzi wa ardhi.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories