Odinga ataka uchaguzi wa urais ubatilishwe


Muungano wa Nasa umepuuzilia mbali utetezi wa mawakili wa Rais Kenyatta na wale wa IEBC kuhusiana na uhalali wa uchaguzi huo na kudai kuwa ukarabati ulifanyiwa fomu za matokeo ya uchaguzi zilizonakiliwa katika vituo vya kupigia kura. Mawakili wa Nasa wakitilia mkazo kukosekana kwa nakala 11 000 za fomu hizo siku tano baada ya mshindi wa uchaguzi kutangazwa na kusema kuwa IEBC ilimtangaza Rais Kenyatta kuwa mshindi bila kudhibitisha iwapo idadi ya kura kwenye fomu zote za vituo vya kupigia kura ziliwiana na zile za kujumlisha kura katika maeneo bunge.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Faiza Wanjiru
More by this author