Oktoba 10 ni sikukuu ya Moi Day

Oktoba 10 ni sikukuu ya Moi Day

Siku ya Jumatano Oktoba 10 itakuwa sikukuu baada ya Waziri wa Usalama Dkt. Fred Matiang’i kuafikia agizo la mahakama uliotolewa mwaka jana.

Matiang’i ametangaza haya kufuatia uamuzi wa jaji wa mahakama kuu George Odunga uliotolewa baada ya miaka saba ya kutoadhimishwa kwa sikukuu ya Moi Day.

Hata hivyo hajatoa maelezo ya jinsi siku hiyo itakavyoadhimishwa.  Sikukuu ya Moi Day haijaadhimishwa tangu kupitishwa kwa katiba mpya 2010.

Jaji Odunga katika uamuzi wake Novemba 2017 alisema kutoadhimishwa kwa tarehe 10 Oktoba iliyofahamika kama moi day awali kunakiuka sheria ya sikukuu za kitaifa.

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories