Penye Nia Pana Njia

Baada ya runinga ya Citizen kuangazia taarifa kuhusu msichana mmoja mwenye umri wa miaka 19 anayefanya kazi ya nyumbani eneo la Thika akitumia baiskeli kuzunguka maeneo kadhaa kuchangisha fedha ili kulipa gharama ya matibabu ya hospitali ya mamake ya takriban milioni 1.1. Hatimaye wafadhili wamejitokeza kumsaidia Esther Wairimu. Mamake Esther, Nancy Njeri alifariki tarehe 27 mwezi jana katika hospitali kuu ya Kenyatta baada ya jirani yake kumgonga na mbao kichwani na baada ya kuaga familia yake ilishindwa kulipia gharama hiyo ikiubidi mwili kusalia katika hifadhi ya Hospitali Kuu ya Kenyatta.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories