Peter Kenneth ajitosa tena kuwania ugavana Nairobi, akiwa huru


Mwanasiasa Peter Kenneth hii leo ametangaza rasmi azma yake ya kuwania kiti cha ugavana wa Nairobi kama mwaniaji huru. Kenneth ameelezea kutoridhishwa kwake na jinsi mchujo wa chama cha Jubilee uliendeshwa na kudai kuwa wizi wa kura za mchujo huo ulimnyima nafasi ya kuongoza mji wa Nairobi kwa kitiki ya chama hicho.

Mkakati huu mpya umeafikiwa baada ya mashauriano ya kina na wenyeji wa Nairobi, kenneth amesisitiza.
Kunadhifisha mji wa Nairobi, kuboresha huduma za kimsingi na uwajibikaji ni baadhi ya malengo ya mwaniaji huyo ambaye ameelezea imani yake kuwa wenyeji wa Nairobi watamchagua kuwa gavana katika kinyanganyiro cha uchaguzi mkuu

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: MPs threaten to slash NYS budget

Story By Citizen Team
More by this author