Peter Kenneth atarajiwa kujitosa kinyanganyironi kwenye kiti cha ugavana Nairobi

Aliyekuwa mbunge wa Gatanga Peter Kenneth amejitosa kwenye kinyang’anyiro cha ugavana kaunti ya Nairobi, na kutangaza hatawania Urais mwaka ujao. Kenneth pia amesema chama chake cha Kenya national congress kiko tayari kufungasha virago na kujiunga na kile cha Jubilee. Uamuzi wa Kenneth ukitarajiwa kuvuruga mpangilio wa siasa za jubilee jijini Nairobi, na kitendawili cha atakayepeperusha bendera ya chama hicho mwaka ujao, huku wadadisi wa masuala ya siasa wakidokeza kuwa mbunge huyo wa zamani analenga kumrithi Rais Uhuru kenyatta kisiasa, baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Francis Gachuri ana taarifa kamili.

Tags:

governor

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories