Rais Kenyatta afungua kituo cha kutibu saratani


Wanaogua saratani sasa wamepata afueni baada ya kuzinduliwa kwa mashine mpya ya matibabu katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta. Hospitali hiyo sasa ikiwa na mashine tatu za matibabu na moja zaidi ya uchunguzi, muda wa kusubiri matibabu sasa utapungua kutoka miezi mitatu hadi mwezi mmoja. Aidha wagonjwa 190 wataweza kutibiwa kila siku.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Faiza Wanjiru
More by this author