Rais Kenyatta aimarisha ngome yake Muranga

Rais Uhuru Kenyatta amepuuzilia mbali madai ya kinara wa NASA Raila Odinga kuwa majeshi yanapangiwa kutumiwa kuiba kura. Katika ziara yake huko Murang’a, rais amemkashifu Raila kwa kuingiza siasa katika masuala ya usalama na kumtaja kama ambaye ananuia kuleta mgawanyiko wa kikabila. Rais Kenyatta amesema kuwa mafunzo yanayotolewa kwa maafisa wa usalama kwa sasa yanahusisha maafisa kutoka pembe zote za nchi na   yanahusiana na mikakati ya kiusalama wakati wa uchaguzi.

Tags:

Uhuru kenyatta JUBILEE muranga kembi Gitura

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories