Rais Kenyatta aongoza maadhimisho ya mwaka wa 39 tangu rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta kufariki


Rais Kenyatta aongoza maadhimisho ya mwaka wa 39 tangu rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo ...

Rais Uhuru Kenyatta hii leo ameongoza nchi katika kufanya maadhimisho ya mwaka wa 39 tangu Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta, kufariki mnamo tarehe 22 mwezi Agosti mwaka 1978.

Katika hafla iliyoandaliwa katika kanisa la mtakatifu Stefano jijini Nairobi, rais Kenyatta aliwahimiza wakenya kuungana ili kulijenga taifa kama waanzilishi wetu walivyokusudia.

Aidha Naibu wake, William Ruto, aliapa kuwa serikali ya Jubilee itaendeleza misingi ya utangamano katika makabila yote 44 za kenya.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Jacques Masea
Story By Jacques Masea
More by this author