Rais Kenyatta azindua sehemu ya pili ya SGR

Rais Uhuru Kenyatta hii leo amekashifu wale wanaopinga mradi wa pili wa kujengwa kwa reli ya kisasa kuelekea Naivasha kutoka Nairobi na kusema kuwa swala la reli kupita katikati mwa Mbuga ya Nairobi itashughulikiwa ipasavyo. Rais Kenyatta aliyasema haya alipozindua mradi wa kujengwa kwa reli hiyo katika eneo la Em-bulbul, Ngong kaunti ya Kajiado. Mradi huo umekumbwa na utata huku kesi ikiwasilishwa mahakamani kupinga reli hiyo kupita ndani ya hifadhi ya wanyama ya Nairobi.

Tags:

NAIVASHA SGR

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories