Rais Magufuli akemea ukabila Kenya

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewataka Wakenya kusitisha migawanyiko ya kikabila. Rais huyo ambaye amekuwa humu nchini kwa ziara ya siku mbili, alisisitiza umuhimu wa Wakenya kuwa na umoja kama njia mojawapo ya kukuza uchumi wa taifa.
Wakati wa ziara hiyo, Magufuli na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta walikubaliana kwa kauli mmoja kuanzisha ujenzi wa barabara mbili zinazounganisha Kenya na Tanzania ambazo zitarahisisha usafiri na uchukuzi wa bidhaa.

Tags:

ukabila Rais John Pombe Magufuli

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories